Mtoto Lu Hao ana umri wa miaka 4 na uzito wa kilo zaidi ya 60 ambayo ni zaidi ya mara tano ya uzito wa watoto wa kawaida.
Baba na mama wa mtoto huyo anasema mtoto wao aliongezeka uzito mara baada ya miezi mitatu tangu azaliwe,ambae mtoto huyo alizawaliwa na uzito wa kawaida tuu.
Wazazi hao wamelalamika kuwa kila njia wanayotumia katika kuhakikisha mtoto huyo anapungua zimeshindikana na matokeo yake mwaka uliopita aliongezeka kilo 10 zaidi badala ya kupungua.
Lu Hao huwa anatembea na wazazi wake kila siku ili kuhakikisha anapata mazoezi ili kuimarisha afya yake.Lu Hao ambae hapendi kutembea kwenda shule ambae huwa anatumia baiskeli kwa kuwa mama yake hawezi tena kumbeba.Mama wa mtoto huyo ansema inawabidi wa mpe chakula cha wastani kwani huwa anakula chakula zaidi na akinyimwa huwa analia na kusumbua.Ili kuhakisha mtoto huyo anapungua wazazi wake wamemjengea sehemu ya kuchezea mpira wa kikapu na kumchukua kuogelea mara kwa mara.Wazazi wa mtoto huyo wamempeleka hospital tofauti katika kupata ushauri wa madaktari kujua ni jinsi gani wanaweza kumsaidia mtoto wao kwani wanahofia moyo wake kushindwa kufanya kazi vizuri kutokana na muongezeko wa uzito wake.
No comments:
Post a Comment