Thursday, October 11, 2012

Charlie Chaplin aliwahi kushindwa kwenye shindano la kumfananisha

Charlie Chaplin mchekeshaji muigizaji maarafu duniani inadaiwa alishindwa kwenye shindano hilo la watu waliofanana nae lililokuwa linasimamiwa na kaka yake.Kwa lugha ya kingereza tunasema look alike contest.
Alikuwa maarufu sana katika kucheza filamu au vichekesho vya kimya-kimya (ambapo zilikukuwa hamna kuongea wala sauti). Aliigiza, aliongoza, alizipanga script na kuziongoza filamu zote zilizokuwa zinamhusu.
 Charlie Chaplin alikuwa akifanya kazi hizo takriban kwa miaka 70, alianza akiwa na umri wa miaka mitano, na mpaka ilipofika miaka 80. Sehemu husika alizokuwa akicheza Charlie Chaplin maranyingi iliitwa "the Tramp". Tramp alikuwa mtu mwenye heshima zake, ambaye amevaa koti, suruali likubwa, viatu na kofia nyeusi huku akichekesha watu.

No comments:

Post a Comment