Thursday, February 17, 2011

Tamthilia ya Kiafrika inayoiteka Dunia

Ni tamthilia inayokwenda kwa jina la The No. 1 Ladies' Detective Agency ambayo iko Botswana imefanikiwa kuonekana Dunia kote kutokana na kazi yake nzuri inayofanya ikiwemo na kufuata maadili mazuri ya Kiafrika.
Ni tamthilia inayo fundisha watu mbalimbali duniani maadili mazuri ya Kiafrika.Tamthilia hii inaonyeshwa na kituo cha tv cha HBO ambacho ni kituo ambacho kinarusha matangazo yake duniani kote.
Tamthilia hii inatufundisha haswa sisi waafrika kuwa kazi nzuri huonekana na jitihada ufanikiwa kutokana na kazi hio.Jamii nyingi haswa za Kiafrika zimekuwa na tabia ya kufata maigizo ya nchi za nje yaani kuanzia uigizaji,maadili yao na kufanya movie zao kuwa zenye picha ambazo hazistahili haswa kwa jamii yetu ya kiafrika.Tufanye kazi bora na si bora kazi.


No comments:

Post a Comment